HabariPilipili Fm

Bunge La Kaunti Ya Mombasa Kurejelea Vikao Vyake .

Bunge la kaunti ya Mombasa limeratibiwa kurejelea vikao vyake adhuhuri hii leo baada ya kutoka likizo ya Idd Ul Fitri.
Vikao hivyo vilivyositishwa tarehe tano mwezi huu vinarejelewa, huku mjadala mkuu ukiwa ni ule wa kumwondoa spika wa bunge hilo Thadius Rajwai, mswada uliotayarishwa na mwakilishi wa Tudor Patrick Simiyu.
Hata hivyo, kuna ati ati ya kuendeshwa kwa mjadala huo, ikizingatiwa  kuna amri ya mahakama ya Mombasa iliyoamrisha mjadala huo kutojadiliwa hadi baada ya siku 12 kukamilika.

Show More

Related Articles

Close