BurudaniPilipili Fm

Ijue Safari Ya Mziki Ya Susumila.

Yusuf Kombo almaarufu Susumila ni msanii ambaye alizaliwa miaka 33 ilyopita katika  eneo la Chumani kaunti ya Kilifi na mafanikio yake ya kimziki yamemfanya kuwa mmoja kati ya wasanii tajika kanda ya pwani na kenya nzima kwa ujumla.

Susumila alianza mziki back in  2000 na ngoma yake ya kwanza ilyompatia mafao mkubwa ilikua ni Siasa Duni aliyoitoa mwaka 2007 ni ngoma iliyozungumzia maswala nyeti ya uongozi na wanasiasa.

Baada ya hapo msanii huyu hakukoma kudondosha ngoma kwani baada ya siasa duni aliachia Ngangari Kinoma ambayo pia ilipata airplay kote si kwa matatu radio na disco vumbi.

Hadi kufikia sasa msanii Susumila ana zaidi ya nyimbo ambazo zingekua zinaekwa kwa mfumo wa album basi zingefika zaidi ya album nne.

Susumila aka Nugu alishawahi kufanya collabo mbili na Chikuzee za ngoma itambae na hidaya ngoma ambazo zilimpatia upeo na kumuongezea sifa, ngoma hizo zilizalishwa na producer mkali afrika mashariki TK2 katika studio za Hornet ambayo baadaye ilikuja ikasambaratika.

Pia ameshawahi kufanya collabo ya Kide kide na Bangereba rmx na msanii Dazlah Kiduche.

Bingwa huyu wa mziki anasifika kwa kuvalia mapete mikononi mwake na pete yaghali anayoivaa kwa sasa ilimgharimu shilingi elfu 38.

Safari ya mziki kwake haijakua rahisi kwani ashahusishwa na madai ya kujihusisha na ushirikina na hata kusemekana kuwaroga baadhi ya wasaniii wenzake jambo ambalo alijitenga nalo.

“Mimi bidii ndio iliyonifikisha hapa na kama watu wanadhani uchawi ndio suluhu basi wakaroge pia wao wafanikiwe ila mimi naamini Mungu na bidii na heshima kwa kila mtu hususani mapresenters,maDjs,mafans na washkadau wote kwenye music indutsry “.Alisema Susumila.

Itakumbukwa ni mwaka jana ambapo aliachana na mama watoto wake Ruth ambaye walitofautiana na hakusita kutafuta ubavu wake kwani miezi kadhaa alifanya nkaha kubwa akihalalishwa kumuoa Kibibi salim mmoja wa waigizaji bora kutoka humu nchini na sasa wanaishi rasmi kama mke na mumewe.

Nguli huyu wa mziki amekuwa akiendelea kuijenga himaya yake ya mziki na yeye ndo mwanzilishi wa mishe mishe music empire.

Kwa sasa anatamba na nyimbo ya mapepe aliomshirikisha king kaka kutoka Nairobi  na mwezi ujao anatarajiwa kuzindua ujio wake mpya ambao pia inaaminika atachange lebel yake ya mishe mishe music empire.

Kwenye mahojiano na meza ya shhhhhh…123 msanii susumila alisema majina ya empire yamekua mengi hivyo anataka kujibrand upya.

“Nataka kujibrand upya na mwezi wa nane tarehe nane nitazindua mambo mapya hivyo mashabiki wakae mkao wakula kwa ujio wangu mpya na lebel mpya”. Alisema Susu

 

 

Show More

Related Articles

Close