HabariPilipili Fm

Kaimenyi Awataka Wanasiasa Kutotumia Swala La Ardhi Kujipa Umaarufu

Wizara ya ardhi kwa ushirikiano na tume ya ardhi nchini imeweka mipangilio mwafaka ya kuona kuwa maswala ya mizozo ya  ardhi humu nchini  hayatumiwi  na wanasiasa kujitafutia kura na umaarufu.

Imebainika kuwa   kwa miongo mingi viongozi wengi wa kisiasa humu nchini huchukulia dhulma za  kihistoria za ardhi miongoni mwa wananchini haswa wa eneo la pwani kama chambo cha kujipatia vyeo.

Waziri wa ardhi Prof Jacob Kaimenyi ameikagua afisi ya ardhi ya kaunti ya Kwale nakusema wameweka mikakati ya kutoa hati miliki za ardhi milioni tatu kwa wananchi kufikia  mwaka ujao wa uchaguzi mkuu wa  2017 kama njia moja wapo ya kuwaepusha wananchi na danganya toto za viongozi wa kisiasa.

Aidha waziri ameitaka serikali kutenga fedha zitakazowawezesha kuwasaidia maskwota kupata makao ya kudumu  kwa mjibu wa sheria.

 

 

 

Show More

Related Articles

Close