MichezoPilipili Fm

Mchezaji Wa Brazil Afeli Majaribio Kilabuni Gor Mahia.

Mabingwa wa ligi kuu humu nchini Gor Mahia sasa ni rasmi hawatamsajili mshambulizi kutoka Brasil Thiago De Lima.

Mbrasil huyo amekua akifanya mazoezi na mabingwa hao akitarajia kupata mkataba lakini kulingana na benchi la kiufundi la timu ya Gor nikuwa mshambulizi huyo hana ubora wa viwango vya kuichezea timu hio na hakuweza pia kumridhisha mkufunzi Ze Maria na sasa ameambiwa anaweza kuondoka kilabuni hapo kurudi zake Brasil.

Taarifa ya Gor inasema ni kweli alifanyiwa majaribio lakini kilabu imeshindwa kumpa mkataba kwani hana viwango.

Inasemekana mchezaji huyo alishindwa kumridhisha mkufunzi toka siku ya kwanza na sasa Gor inapania kumrudisha Meddie Kagere kilabuni hapo wakati wowote.

Kuondoka kwa De Lima kunarudisha kumbukumbu za mbrasil mwengine Geovanni Rodriguez ambaye alirudi kwao mnamo mwaka wa 2013 kwa kushindwa kumridhisha mkufuzni Zdravko Logarusic

Show More

Related Articles

Close