HabariPilipili Fm

Mihadarati Yaumiza Vijana Taita Taveta.

Matumizi ya mihadarati miongoni mwa baadhi ya vijana kaunti ya Taita Taveta yametajwa kuathiri pakubwa hatua zao za kimaendeleo.

Mwakilishi wa vijana kaunti hiyo Felton Mwashighadi, anasema idadi kubwa ya vijana wanaojihusisha na mihadarati eneo hilo hawajajiendeleza kimaisha licha ya serikali ya kaunti na ya kitaifa kubuni vitengo vya kupeana fedha za mikopo kwa vijana.

Sasa anawahimiza vijana wanaozembea na kujihusisha na utumizi wa mihadarati kaunti hiyo, kuwajibika kikamilifu ili waboreke kimaisha.

Show More

Related Articles

Close