MichezoPilipili Fm

Mji Wa Mombasa Kuandaa Michezo Ya Wajumbe Wa Afrika Mashariki.

Mji wa Mombasa umebahatika kuandaa mashindano makubwa ya wabunge wa jumuia ya afrika mashariki mwezi disemba mwaka.

Wakizindua rasmi mikakati na mipango kabambe kuhusiana na michuano hiyo itakayojumuisha wajumbe zaidi ya elfu moja kutoka mataifa wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki katika afisi ya kamishna wa kaunti ya Mombasa,wabunge hao  wakiongozwa na mwenyeji wao seneta mteule wa kaunti ya kilifi Mvita Mshenga wamewataka wananchi kujitayarisha kwa michuano ya kihistoria na pia kuwahimiza kujitokeza kwa wingi wakati wa michuano hiyo ya kipekee.

Kuhusiana na maswala ya usalama kamishna wa kaunti ya Mombasa Maalim Mohamed amewahakikishia wajumbe hao pamoja na wageni watakaokuja kushuhudia michuano usalama wakutosha

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila baada ya miaka saba yatajumuisha michezo yote mikuu ikijumuisha kandabda,volibali,mpira wa vikapu, raga, golf,riadha,pamoja na masumbwi na uogeleaji.

Show More

Related Articles

Close