HabariPilipili Fm

Watekajinyara Wafikishwa Mahakamani Mombasa.

Afisa mmoja wa polisi wa kitengo cha utawala amefikishwa mahakamani mjini Mombasa, akikabiliwa na mashtaka ya utekaji nyara.

Inaarifiwa Timothy Nganyi mnamo tarehe sita ya mwezi huu katika gatuzi dogo la likoni akiwa na Rosemary Ngina ,Khamis  Juma na aliyekuwa mwanajeshi wa kdf Nassir Ochieng,  kwa pamoja wakitumia garia aina ya probox walimteka nyara Abdalla Rashid kulingana na mashtaka yaliyosomwa mahakamani,wanne hao walitumia ulaghai wakitaka 70,000 mwathiriwa ili waweze kumuachilia.

Wote wamekanusha mashtaka dhidi yao mbele ya hakimu Julius Nang’ea.

Inaaminika wamekuwa pia wakihusika na msururu wa visa vyengine vya uhalifu huku ikiaminika huenda wakakabiliwa na mashtaka mengine.

Washtakiwa wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja na wapate mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Kesi itatajwa mnamo tarehe ishirini ya mwezi huu ,kwa mwelekeo zaidi.

Show More

Related Articles

Close