HabariPilipili Fm

Serikali Za Kaunti Za Onywa.

Mshirikishi wa serikali kuu kanda ya Pwani Nelson Marwa amezionya serikali za kaunti dhidi ya kudandia miradi ya serikali kuu na kudai miradi hiyo ni yao.
Marwa amesema serikali za kaunti zimekuwa zikitenga fedha kwa lengo la kufanya miradi huku wakitumia wakitumia miradi ya serikali kuu kujisifia kama yao.
Marwa amesema hali hii inaleta mkanganyiko miongoni mwa wakenya wasijue midair gani ni ya serikali kuu nay ale ya serikali za kaunti.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mbunge wa Kilifi kaskazini Gedion Mung’aro ambae maesema imekuwa tabia ya serikali za kaunti kudandia miradi ambayo sio yao.

Show More

Related Articles

Close