HabariPilipili Fm

Tavevo Yakanusha Madai Ya Kuongeza Ada Za Ulipaji Maji.

Bodi ya kampuni ya Tavevo inayohusika na usambazaji maji kaunti ya Taita Taveta, imepuuza madai kwamba baadhi ya wakaazi kaunti hiyo hupokea bili za matumizi ya maji kutoka kwa kampuni hiyo, zisizoambatana na matumizi yao.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Mohammed Washalla, anashikilia kuwa maafisa wa kampuni hiyo wana ujuzi wa kutosha na kwamba wanafuata utaratibu ufaao katika utendakazi wao.

Hata hivyo amesema kuna haja ya wasioridhia bili wanazopokea, kuwasilisha lalama zao kwa afisi husika ili wapate muafaka.

Kumekuwa na madai kwamba baadhi ya maafisa wa kampuni hiyo huzembea katika utendakazi wao, huku wakipeana bili za maji kwa kukadiria kabla ya kuchukuwa hatua ya kusoma kiwango kamili.

Show More

Related Articles

Close