HabariPilipili Fm

Wengi Waendelea Kuihama CORD

Zaidi ya wafuasi 100 kutoka vyama mbalimbali eneo bunge la Malindi  wametangaza kuvihama vyama vyao na kuapa kukiunga mkono chama cha Jubilee kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Wakiongozwa na Peter Ponda aliyekuwa mgombea wa ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Malindi kwa tiketi ya chama cha Uzalendo wafuasi hao wameipongeza serikali iliyopo mamlakani inayoongizwa na Rais Uhuru Kenyatta kwa kuleta maendeleo humu nchini.

Ponda aidha amekashifu vikali hatua ya baadhi ya viongozi hapa Pwani wanaounga muugano wa CORD huku wakimtaja kinara wao Raila Odinga kama kiongozi anayejali maslahi yake binafsi badala ya wananchi wengine.

Amesema watamuunga mkono mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mungaro katika azma yake ya kuwania kiti cha ugavana kwenye uchaguzi ujao huku akiutaja muungano wa Jubilee kuwa wenye manufaa katika uongozi serekalini.

Show More

Related Articles

Close