HabariMilele FmSwahili

Watu 20 wakimbizwa hospitalini baada ya kudaiwa kula Githeri yenye sumu Baringo

Wakulima 20 wamelazwa katika hospitali ya Kabarnet kaunti ya Baringo baada ya kula githeri inayoshukiwa kuwa ya sumu. 4 kati yao wanaarifiwa kuwa katika hali mahututi na wanapokea matibabu katika hospitali ya Marigat, aliyewapikia chakula hicho cha sumu anasakwa.

Wakulima hao 20 wakiwa wamejihami kwa vifaa vyao vya upanzi walikuwa wamesafiri kutoka kijiji cha Elchamus Kabarnet hadi eneo la Eltebes, Baringo Kusini kusaka mkate wa kila siku

Mkate huu ukigeka kuwa sumu mwendo wa saa nne walipopewa kiamsha kinywa kabla ya kuanza kazi

Kulingana na waliopiga kamsa kuhusu hali hii, wakulima 14 kati ya 20 walipatkana chini ya mti wakilalamikia mauvivu tumboni.

Wasamaria wema wakishirikiana na shirika la msalaba mwekundu, wanasema chakula waliokula  chakula hicho walilalama kilikuwa kinatoa uvundo.

Show More

Related Articles

Close