Biashara

Wafanyibiashara Wundanyi Walalamikia Usimamizi Duni Wa Soko.

Wafanyibiashara katika soko la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta sasa wanalalamikia usimamizi wa soko hilo pamoja na serikali ya kaunti kwa mazingara duni yakufanyia kazi.
Wafanyibiashara hao wanasema wamekua wakipitia hali ngumu nyakati za mvua, kutokana na maji ambayo huingia kwenye soko hilo na kulemaza biashara kutokana na ukosefu wa mitaro ya kupitishia maji.
Wakati huo huo wamelalamikia tatizo la kukatizwa kwa nguvu za umeme mara kwa mara, swala linaloathiri shughuli zao nyakati za usiku.

Show More

Related Articles

Close