HabariMilele FmSwahili

Mwangi Kiunjuri atemwa kama waziri katika mabadiliko yaliyotangazwa na Rais

Mwangi Kiunjuri na Adan Mohammed wametemwa kama mawaziri wa kilimo na viwanda mtawalia. Katika mabadiliko yaliotangazwa na rais Uhuru Kenyatta,Mutahi Kagwe sasa ndiye waziri wa afya,Bet Maina ni waziri wa viwanda na John Weru ni waziri wa biashara.

Akihutubu kutoka Ikulu ya Mombasa, Rais Uhuru Kenyatta ametetea mabadiliko hayo akisema yanalenga kuboresha utoaji huduma kwa wakenya.

Mwangi Kiunjuri ambaye amekua mwandani wa naibu Rais William Ruto akitemwa kama waziri wa kilimo sawa na Adan Mohammed kutoka wadhfa wa waziri wa masuala ya Afrika Mashariki.

Katibu wa viwanda Betty Maina sasa ndiye waziri mteule wa viwanda naye aliyekua seneta wa Nyeri Mutahi Kagwe sasa ndiye waziri mteule wa afya.

Ukuru Yattani ambaye amekua kaimu waziri wa fedha sasa atashikilia wadhfa huo kikamilifu, Rachael Omamo sasa ni waziri wa masuala ya kigeni akihamishwa kutoka kuwa waziri wa ulinzi, wadhfa ambao sasa utashikiliwa na Monica Juma.

Sicily Kariuki ni waziri wa majRi akihamishwa kutoka wizara ya afya, Peter Munya ni waziri wa kilimo akihamishwa kutoka wizara ya biashara,Simon Chelugui ni waziri wa leba akihamishwa kutoka wizara ya maji.

Kutemwa kwa Kiunjuri kunafikisha tamati,hali ya hati hati ambayo imekua maishani mwake tangu alipojiunga na wizara ya kilimo ambapo mara si moja ameshtumiwa kwa kuzembea na kuruhusu matapeli kuiteka nyara wizara hiyo.

Aidha,Kirimi Kaberia amehamishwa kama katibu wa wizara ya michezo na sasa ni katibu wa wizara ya madini,John Weru ni katibu mteule wa biashara,Solomon kitungu katibu mteule wa uchukuzi.

Waliopendekezwa kuwa mawaziri na makatibu wapya watasubiri kupigwa msasa na wabunge kabla ya kuidhinishwa kuhudumu

Show More

Related Articles

Close