HabariMilele FmSwahili

Msako mkali dhidi ya wanaouza unga uliopigwa marufuku Bomet waanzishwa

Msako mkali umeanzishwa kaunti ya Bomet dhidi ya wafanyabiashara wanaoendelea kuuza unga uliopigwa marufuku.

Kamanda wa polisi Naomi Ichami anasema wameendesha misako baada ya kuibuka madai kuwa kuna baadhi ya wafanyabaiashara ambao bado wanauza unga wa dola uliokuwa miongoni mwa uliopigwa marufuku.

Aidha amewataka wenyeji kuwa waangalifu ili wasilaghaiwe,akionya hatua kali dhidi ya watakaopatikana wakiuza bidhaa hizo.

Misako sawia inaandaliwa kaunti ya Kilifi, wenyeji pia wakitahadharishwa dhidi ya kunua unga uliopigwa marufuku wakionywa kuhusu afya yao

Show More

Related Articles

Close