HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa KCPE waendelea kusherehekea kote nchini

Familia na jamaa za wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani  wa KCPE bado zinasherehekea ushindi wao. Katika kituo cha kurekebisha tabia cha Makadara hapa Nairobi ilikuwa furaha isiyokuwa na kifani baada ya kijana mmoja aliyekuwa wa kurandaranda kupata alama 410 katika mtihani huo. Simon Kirungu akiwa miongoni mwa watoto 164 wa kurandaranda mitaani walioufanya mtihani huo

Mjini Mombasa, wazazi na jamii imejitoekza kusheherekea mwanafunzi bora kutoka pwani aliyesomea shule ya msingi ya Navy. Chaka Derrick Mweru akipata alama 435 kwenye mtihani huo.

Emmaculeta Baraka kutoka shule ya umma ya Bungoma DEB naye akishindwa kuficha furaha yake kwa kuwa mwanafunzi bora aliyepata alama 419.

Huko  Mumias Jumla ya wanafunzi 6251 walifanya mtihani Mumias Magharibi.

Mwanafunzi bora akiandikisha alama 425

Show More

Related Articles

Close